Friday, May 30, 2008

Salaam!

Habari za leo ndugu zangu.
Mnaoistahili shkamoo yangu nawasalimia.
Hiyo post hapo chini najua itawachekesha wengi, kama mjuavyo mimi ni miongoni mwa wanyakyusa wachache mno raia wa moshi kwa kuzaliwa na Dar es salaam kwa makazi ambaye naweza kuongea kinyakyusa kizuri na kilichonyooka kwa kiasi hicho.

Anyways lengo la blog hii ni kama linavyoonekan pale juu. Idea ilitokea kwenye kikao cha kuvunja kamati ya send off ya dada yangu Irene kilichofanyika pale kinondoni karibu na usalama wa taifa. ikaonekana ni neno jema kama tutakuwa na kaushirikiano kadogo ambako katakuwa na lengo la kutusaidia pale tunapoata dharura, sherehe au hata kupongezana mara walau mara moja au mbili kwa mwaka kwa mfano mwaka mpya! ujue sisi wengi hapa Dar kukutana ni Dharura!!! maana maisha yamwkuwa tight mpaka tunasahau hata kupigiana simu!! basi chama hichi kitusaidie kufahamiana na kusaidiana.

nimeona ushirikiano kama huu nnaotaka kuanzisha ukikua mpaka ukawa SACCOS na sasa wamwanza hata kuwekeza sehemu sehemu! kwa hiyo manufaa yake ni makubwa kama tukiwa serious kwa maana ya kushirikiana katika mawazo,hali na mali. pia nimeona ushirikiano kama huu ukifa kwa kutwatu kutokuwa serious,kwangu mimi,kuliko tuanzishe kitu kitakachokufa bora tusianzishe kabisa!!

napokea mawazo na ushuri kupitia email yangu (angalia post ya kinyakyusa hiyo hapo chini) au kupitia coments zenu mtakazoweka kwenye post hizi.

mwisho kabisa nawaahidi ntakuwa hapa kuwaletea habari zte zinazojiri miongoni mwetu iwe njia rahisi kufikika ya mawasiliano. nategemea ushirikiano wenu.

Wasalaam.

Ntimi Mololo

No comments: